Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amesema watu wenye matatizo ya moyo, wajawazito na wenye maradhi ya kidole tumbo ambao ni wanachama watapata faraja baada ya gharama za matibabu ya magonjwa hayo kujumuishwa kwenye bima zao.
NHIF imetangaza kuhudumia upasuaji wa moyo kwa viwango vyote pamoja na wa uzazi na ule wa kidole tumbo ambavyo awali havikujumuishwa kwenye bima.
Konga amesema jana kuwa uanzishwaji wa huduma hizo utaongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za afya.
“Awali, wagonjwa walikuwa wakichangia gharama siku ya kwanza wanapomuona daktari na wanapokwenda mara ya pili, walitakiwa kulipa gharama ileile, bila kujali ni mara ngapi watatakiwa kumuona,” amesema na kuongeza kwamba malipo hayo sasa yatafanyika mara moja tu ya kwanza.”


ConversionConversion