UKUʻALOFA, TONGA: Waziri wa Mambo ya Ndani na Michezo wa Serikali ya Visiwa vya Tonga, Fe’ao Vakata, ameshinikizwa kujiuzulu baada ya kumrushia ‘glass’ ya mvinyo mmoja wa watumishi waandamizi katika ofisi yake.
Fe’ao Vakata.
Tayari Waziri Mkuu wa Tonga, Akilisi Pohiva, amethibitisha kuenguliwa kwa waziri huyo akisema tabia yake hiyo isingeweza kuvumiliwa.
Pohiva alisema baada ya kuwapo kwa shinikizo la kutaka waziri huyo ajiuzulu, binafsi alifanya mawasiliano na mfalme kuomba ili aridhie kutengua uteuzi wa waziri huyo.
Akizungumzia tukio la waziri wake huyo, Pohiva alisema Vakata alishindwa kudhibiti hasira zake na kwamba, hata hivyo, hiyo si sababu inayojitosheleza kumshambulia mtumishi wa umma.
“Ukiwa waziri unahitajika kulinda hadhi yako, unahitajika kuwajibika, kuwa na kiwango cha juu cha maadili. Kinyume cha hapo, ukishindwa kumudu kuishi katika misingi hiyo, basi hakuna njia nyingine ni kukuondoa tu. Huyu waziri amevuka mipaka ya uadilifu kutokana na kitendo hiki cha aibu alichofanya.” alisema na kuongeza kwamba atafanya uteuzi wa waziri mwingine mpya, baada ya kurudi kutoka katika ziara yake New York, Marekani.
Waziri Vakata alizaliwa Februari 13 mwaka 1969 ni mwanasiasa ambaye pia ni mbunge katika Bunge la Tonga. Ni msomi wa shahada ya umahiri katika sayansi ya fizikia na kocha wa kiwango cha cheti katika mchezo wa ragbi.
Amewahi kufundisha katika shule za sekondari na vile vile kuwahi kufanya kazi serikalini akiwa ofisa wa kutoa leseni za radio, chini ya Wizara ya Mawasiliano.
Julai mwaka 2012, Vakata aliwahi kukumbwa na kashfa ya kufuja fedha za serikali akiwa katika ziara ya ‘kulazimisha’ Australia, alilazimika kurejesha fedha hizo alizofuja.
Fe’ao Vakata.Tayari Waziri Mkuu wa Tonga, Akilisi Pohiva, amethibitisha kuenguliwa kwa waziri huyo akisema tabia yake hiyo isingeweza kuvumiliwa.
Pohiva alisema baada ya kuwapo kwa shinikizo la kutaka waziri huyo ajiuzulu, binafsi alifanya mawasiliano na mfalme kuomba ili aridhie kutengua uteuzi wa waziri huyo.
Akizungumzia tukio la waziri wake huyo, Pohiva alisema Vakata alishindwa kudhibiti hasira zake na kwamba, hata hivyo, hiyo si sababu inayojitosheleza kumshambulia mtumishi wa umma.
“Ukiwa waziri unahitajika kulinda hadhi yako, unahitajika kuwajibika, kuwa na kiwango cha juu cha maadili. Kinyume cha hapo, ukishindwa kumudu kuishi katika misingi hiyo, basi hakuna njia nyingine ni kukuondoa tu. Huyu waziri amevuka mipaka ya uadilifu kutokana na kitendo hiki cha aibu alichofanya.” alisema na kuongeza kwamba atafanya uteuzi wa waziri mwingine mpya, baada ya kurudi kutoka katika ziara yake New York, Marekani.
Waziri Vakata alizaliwa Februari 13 mwaka 1969 ni mwanasiasa ambaye pia ni mbunge katika Bunge la Tonga. Ni msomi wa shahada ya umahiri katika sayansi ya fizikia na kocha wa kiwango cha cheti katika mchezo wa ragbi.
Amewahi kufundisha katika shule za sekondari na vile vile kuwahi kufanya kazi serikalini akiwa ofisa wa kutoa leseni za radio, chini ya Wizara ya Mawasiliano.
Julai mwaka 2012, Vakata aliwahi kukumbwa na kashfa ya kufuja fedha za serikali akiwa katika ziara ya ‘kulazimisha’ Australia, alilazimika kurejesha fedha hizo alizofuja.

ConversionConversion