Watu wasiojulikana wamemvamia na kumjeruhi kwa lengo la kumkata mkono, katibu wa chama cha wenye ulemavu wa ngozi wilayani Nzega, mkoani Tabora Bw Juma Moshi Juma, ambapo aliwazidi nguvu wakakimbia alipoomba msaada, huku wakimwachia majereha kadhaa nyumbani kwake kata ya Mazengo mjini Nzega.Akizungumza nawaandishi wa habari nyumbani kwake baada ya kutoka katika hospitali ya wilaya Nzega alipopatiwa matibabu majeruhi huyo katibu wa TAS Bw, Juma Moshi Juma amesema kuwa, alivamiwa na watu wawili usiku wa kuamkia jana ambapo walimkaba kupitia mgongoni, na katika purukushani za kupambana nao wakaanza kupiga mapanga.
Aidha ameiomba serikali kuwasaidia walemavu wa ngozi, kwa kutoa adhabu kali pale watakapobainika watu wenye nia mbaya ya kuwajeruhi walemavu wa ngozi ili kukomesha vitendo hivyo, kuliko kuficha ukweli, akidai ni sawa na kuwaongezea machungu pale hatua zisipochukuliwa.
Kwa upande wake mganga mfawidhi katika hospitali ya wilaya ya Nzega Dkt Godbress Kiguha, amekiri majeruhi huyo kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali, huku katibu tawala wilaya ya Nzega Bw. Onesmo Kisoka, pamoja na kudai majeruhi huyo alipata michubuko, amesema jeshi la polisi lipo katika uchunguzi.


ConversionConversion