Dar es Salaam. Madereva waliotekwa na askari wa kikundi cha uasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamesema njaa ya watekaji hao ndiyo iliyowqaokowa kirahisi na majeshi ya nchi hiyo.
Mmoja wa madereva hao kumi amesema hayo jana baada ya kuwasili nchini kwa ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) huku kukiwa na vilio, machozi ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofika kuwapokea.
Baada ya kushuka kwenye ndege, madereva hao walipelekwa kwa gari hadi eneo la watu maarufu (V.I.P) ambako mmoja wa madereva hao, Athumani Fadhili alipewa nafasi ya kusimulia tukio zima na kufanya hivyo huku akibubujikwa na machozi.
“Waliorodhesha majina yetu kwa kupitia pasipoti zetu, walihoji taarifa za familia zetu, kama tumeoa au la, huku wanaandika, walitutembeza kila walipohisi majeshi yanawakaribia, hadi siku tulipokombolewa.”


ConversionConversion