Serikali kutokopeshwa dawa MSD

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mtendaji wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Lauren Bwanakunu amesema wanakusudia kuacha kukopesha dawa kwa Serikali.

Bwanamkuu amesema mpango huo utazihusu halmashauri na hospitali zote nchini hadi zitakapolipa deni la Sh21 bilioni.

“Tutawanyima huduma wote wasiotulipa, hiyo inaua mtaji wa taasisi, lazima tutengeneze utaratibu.

“Haya ni maagizo ya Rais John Magufuli kwamba tuhakikishe tunakusanya fedha, Serikali ilete fedha sisi tusambaze dawa ili baada ya miaka miwili fedha hizo zifanye kazi nyingine na mtaji uzunguke,” amesema Bwanakunu.

Amesema hawana uhakika wa kuendeleza huduma hiyo iwapo deni hilo halitalipwa kwa wakati na kuwa,

limesababisha bohari hiyo kukabiliwa na uhaba wa fedha na kushindwa kuagiza dawa kwa wakati.

Waziri ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali ipo katika mchakato wa kulipa deni hilo, huku akizitaka halmashauri kuhakikisha zinalipa.

Previous
Next Post »