Spika ashambuliwa mara sita bungeni


WABUNGE sita wa upinzani jana walimshambulia vikali Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kukosoa hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwasimamisha uanachama wabunge wake wawili hivi karibuni.


Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, chama hicho kilisimamisha uanachama wa Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya na wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Mbali na wabunge hao ambao kusimamishwa kwao na kufukuzwa kunakoweza kutarajiwa hatimaye kutapoteza sifa za kushika wadhifa huo, CUF ilimsimamisha pia Mwenyekiti aliyejiuzulu, Profesa Ibrahim Lipumba.

Ndugai alisema kufukuza Mbunge kutoka uanachama kuna athari za kiuchumi kwa taifa kwa sababu "ni gharama kubwa sana kumpata mbunge mwingine."

Previous
Next Post »