Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ameahidi kufunga mabao wakati Yanga leo itakaposhuka dimbani kukipiga na Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.Tambwe amesema kutokana na ushindani uliopo atajitahidi kuhakikisha anatumia kila nafasi kufunga ili kujihakikishia kutetea tuzo ya mfungaji bora ambayo mpaka sasa amechukua mara mbili akiwa na timu za Simba na Yanga.
“Ushindani umeongezeka sana, hivyo nitatumia kila nafasi nitakayoipata uwanjani kufunga ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuandika historia ya kuchukua ufungaji bora kwa mara pili mfululizo nikiwa na timu yangu hii ya Yanga,” alisema Tambwe.


ConversionConversion