Viongozi wa dini wairuka UKAWA, wadai hawakutumwa na ukawa kumuona Rais




Sheikh wa Mkoa Alhad Salum
Dar es Salaam. Sheikh wa Mkoa Alhad Salum amesema viongozi wa dini hawakutumwa na Ukawa kuomba kuzungumza na Rais John Magufuli bali walisukumwa na maono yao waliyopewa na Mungu.

Amesema si kweli kuwa Rais amewatosa viongozi hao kama inavyoripotiwa kwenye vyomvo vya habari kwani ni siku tano tu zimepita tangu waipeleke barua ya kutaka kuonana naye.

“Tuna imani kuwa Rais Magufuli atazungumza nasi hivi karibuni kwani kahuna Rais ambaye alishawahi kuwadharau viongozi wa dini na akitokea atakuwa katika hali ngumu kwani viongozi wa dini ndiyo viongozi wa wananchi makanisani na mskitini hivyo kuwadharau ni kuwadharau wapiga kura,”amesema Salum.

Ameongeza kuwa kamati ya viongozi ya dini inatarajia kukutana kesho kutwa na endapo Rais atakuwa bado hajawajibu basi watajadili suala hilo kwa kuzingatia msimamo wa Ukawa.
Previous
Next Post »