Waziri mkuu awakemea mahakimu wanaofuta kesi bila sababu , adhabu kali kuwashukia


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Jaji Mkuu wa Tanzania kuwachukulia hatua mahakimu ambao wanafuta kesi bila sababu za msingi na wale wanaotumia muda mrefu kusikiliza mashauri kupita muda maalum uliowekwa.

Mh. Majaliwa ametoa agizo hilo leo mjini Kibaha Mkoani Pwani wakati akizindua Mpango Mkakati wa Mahakama na Mradi wa Maboresho ya Mahakama za Tanzania ambao unalenga kuwasogezea wananchi huduma za Mahakama na kuboresha huduma zake kuwa za kisasa zaidi.

Waziri Mkuu amesema mpango mkakati huo pia utasaidia kuimarisha imani ya wananchi kwa mahakama na pia kuwashirikisha na kuongeza kwamba, wananchi wakiwa na imani na Mahakama itachangia utulivu wa nchi na kuwafanya wafanye shughuli za kimaendeleo na ustawi wa jamii kwa amani zaidi.

Kadhalika Mh. Majaliwa ameishukuru Benki ya Dunia kwa kukubali kuikopesha Tanzania Dola za Kimarekani milioni 65 ambazo zitatumika kutekeleza maboresha hayo ya Mahakama.
Previous
Next Post »