Tanzania imeendelea kukabiliwa na changamoto ya uingizwaji wa bidhaa zilizochakatwa kutoka nje ya nchi ambapo takribani tani 2000 za nyama aina ya nguruwe zimekuwa zikiingizwa nchini huku swala hilo likichangiwa na aina ya mbegu zinazozalishwa nchini kuwa zimepitwa na wakatiWakiongea na Channel ten baadhi ya wafugaji wa nguruwe kutoka katika maeneo mbali mbali nchini ambao wamekutana mkoani morogoro kwa lengo la kuanzisha chama cha ufugaji nguruwe wameeleza mbali na tanzania kuwa na idadi kubwa ya mifugo hiyo changamoto imekuwa ni ubora wa mbegu za wanyama hao wanaozalishwa hapa nchini jambo ambalo linapelekea uingizwaji wa nyama nyingi kutoka nje ya nchi.
Uundwaji wa chama hicho cha wafugaji wa nguruwe TAPIFA umelenga kuwakutanisha na kuwaunganisha kwa pamoja kwaajili ya kutetea maslai yao sambamba na kuongeza uzalishaji na thamani ya nyama ya nguruwe ili kukuza soka lake ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kutegemea uchumi wa viwanda.


ConversionConversion