Dar es Salaam. Baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara ya ghafla katika ofisi ndogo ya makao makuu CCM na gazeti la Uhuru, Mtaa wa Lumumba, viongozi wameandaa vikao kuanzia juzi, na leo wanatarajiwa kufanya cha wakuu wa idara.
Hata hivyo, msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alipoulizwa kuhusiana na vikao hivyo amesema hakuna kikao chochote kilichofanyika juzi wala jana.
“Hakuna kikao cha Kamati Kuu (CCM) wala Sekretarieti iliyoketi siku hizo shughuli zinaendelea kama kawaida,” amesisitiza.
Alipoulizwa kuwapo taarifa za wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Uhuru Publications Limited akiwamo Mwenyekiti wake Adam Kimbisa kuhojiwa kuhusu mambo aliyobaini Rais Magufuli, Sendeka amejibu kwa kifupi: “Tumjadili kwa kipi?”


ConversionConversion