Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi auawa na polisi mkoani Kagera.


Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi mkazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera amekufa baada ya kujeruhiwa kwa risasi wakati akikabilaiana na polisi katika kijiji cha Lugongoni wilayani Uvinza baada ya mtu huyo kurusha bomu la kutupwa kwa mkono lililowajeruhi wananchi wanne pamoja na askari polisi mmoja.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema mtu huyo Yahaya Leopard kamuhanda alirusha bomu alilokuwa nalo mkononi wakati akikimbizwa na polisi pamoja na wananchi ambapo pamoja na kujeruhiwa watu hao, alikamatwa na kupigwa na wananchi ambapo kabla hajafa alieleza kuwa anamiliki silaha aina ya SMG nyumbani kwake katika kijiji cha Lukole Ngara, na polisi walifuatilia na kukuta bunduki moja aina ya SMG, magazine saba na risasi 275.

Amesema watu wanne waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni na kwamba kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya dola wanaendelea na msako wa wahalifu ambao walikuwa wakishirikiana nae.
Previous
Next Post »