Vifaa vya kisasa vyaua ajira za vijana 400 Kisarawe


Dar es Salaam. Zaidi ya vijana 400 wa eneo la Msimbu, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, wamepoteza ajira za uchimbaji mchanga kutokana na kampuni iliyopewa zabuni ya kupeleka mchanga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kudaiwa kutumia vibaya kibali walichopewa.

Vijana hao walilalamika kuwa mzabuni huyo amepewa shimo kwa ajili ya kuchimba mchanga eneo la Msanga kwa ajili ya ujenzi wa JNIA Terminal lll, lakini anauuza.

Pia, wanadai kuwa kibaya zaidi ni kwamba mzabuni huyo anachimba kwa kutumia kijiko, hivyo kushusha bei ya mchanga anaotakiwa asiuuze kutokana na masharti ya kibali chake.

Makamu Mwenyekiti wa wachimbaji mchanga wa Omboza, Kata ya Msimbu, Ally Mshamu alisema vijana hao wapo eneo hilo tangu mwaka 2011 wakitumia chepe kujaza mchanga kwenye magari, lakini hivi sasa kazi imekuwa ngumu kwani magari yanatumia kijiko cha mzabuni huyo kujaza mchanga.

Mwekezaji Suleiman Malekela alisema hawafanyi biashara sababu wana bei ya chini ya bei ambayo ni elekezi ya Sh70,000 kwa lori la tani saba.
Previous
Next Post »