Dar es Salaam. Ni miaka saba imepita tangu ushahidi uliotolewa na mshitakiwa wa 12, Koplo Rajabu Hamis Bakari kwenye kesi ya mauaji ya wafanyabiashara, kuonyesha dalili za mwanzo za kumtia hatiani Christopher Bageni ambaye juzi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama ya Rufani.Koplo Bakari akitoa ushahidi mahakamani mwaka 2009 alikiri alivyoshuhudia mauaji ya wafanyabiashara hao watatu kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam yaliyotokea mwaka 2006 kwenye msitu wa Pande chini ya usimamizi wa Bageni, aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni.


ConversionConversion