Dar es Salaam. Meya wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, Hussein Ruhava (ACT-Wazalendo) amesema safari yake ya kikazi aliyofanya nchi Marekani imefungua milango ya fursa mbalimbali kwa manispaa yake na Taifa kwa ujumla.Ruhava ambaye aliingozana na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP), amesema kuwa mkutano huo utaleta maarifa mapya, kupanua fursa za biashara, mitaji mipya kutoka nje ya nchi na kutanua utalii wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.
Pia, Meya huyo amesema Kigoma- Ujiji ambayo ilikuwa miongoni mwa manispaa 15 zilizopata nafasi ya kushiriki mkutano huo, imeazimia kutumia maarifa hayo kuweka mpango mkakati wa kusimamia na kuboresha sekta ya afya, maji, elimu, ardhi, uwazi katika bajeti na uwazi katika takwimu.


ConversionConversion