Mchezo wa EPL uliokuwa unawakutanisha majogoo wa jiji Liverpool dhidi ya wenyeji wao Chelsea ya London katika uwanja wao wa Stamford Bridge katika mechi hiyo Chelsea walikubali kufungwa goli 2-1 dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp, Chelsea walichukua dakika 19 kuruhusu magoli mawili yaliowafanya wakose point tatu wakiwa nyumbani, Dejan Lovren ndio alianza kupachika goli la Liverpool dakika ya 17.Jordan Henderson akapachika goli la pili dakika ya 36, goli pekee la Chelsea lilifungwa na Diego Costa dakika ya 62, hii ni mara ya pili mfululizo kwa Chelsea kuruhusu kufungwa na Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani kwa mechi za Ligi Kuu.


ConversionConversion