Serikali imepanga kutumia kiasi cha Shilingi Billioni 238 katika utekelezwaji wa mpango wa maboresho wa huduma za mahakama nchini jambo ambalo litaongeza ubora wa utoaji haki na usikilizwaji wa mashauri.Akiongea na waandishi wa habari hii leo Jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Mohamed Chande Othman amesema maboresho hayo yataenda sambamba na kuongeza Mahakama Kuu 7, uanzishwaji wa mahakama za wilaya 108 katika wilaya 28 na Mahakama za mwanzo ili kuwawezesha watanzania millioni 21 ambao wanatokea katika maeneo ambayo hayana mahakama hizo kupata huduma.
Mpango huo utakaotekelezwa ndani ya miaka 5 utaanza rasmi baada ya kuzinduliwa tarehe 21 mwezi huu na Waziri Mkuu wa Tanzania Kibaha mkoani Pwani ambapo mahakama hiyo itakuwa na uwezo wa kuendesha shuguli zake kwa muundo wa mahakama za kimataifa ikiwa ni mwanzo wa utekezwaji wa maboresho hayo na dira ya kufikia malengo matatu yenye matokeo makubwa 17 katika uendeshwaji wa mahakama nchini.
Jaji Mohamed Chande Othman amesema, tayari 'Mahakama ya Mafisadi' imeanza kufanya kazi yake kutokana na kukamilika kwa sheria na kanuni za uendeshwaji wa mahakama hiyo ikiwa na majaji 14 huku namna ya kuwalinda mashahidi wa kesi hizo ukizingatiwa.


ConversionConversion