Dodoma. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanza ujenzi wa ofisi yake mjini hapa nyuma ya ukumbi wa mikutano wa CCM (DCC).Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa alisema jana baada ya kutembelea kiwanja hicho, kuwa ujenzi wa ofisi hiyo utakamilika mwaka 2018.
Kamishna wa Sensa na Makazi, Amina Said alisema wamepanga kujenga jengo la ghorofa sita kulingana na ramani iliyotakiwa kutumiwa kujengea ofisi hiyo jijini Dar es Salaam, lakini baada ya kauli ya Rais John Magufuli ya kuhamishia ofisi zote za Serikali Dodoma, wanalazimika kulijenga jengo hilo mkoani humo.
Hata hivyo, alisema wanaweza kubadilisha au kuongeza ghorofa nyingine kulingana na ushauri wa wataalamu.


ConversionConversion