Ni utamaduni kuwapa majina watoto pindi wanapo zaliwa, baadhi ya wazazi huwapa majina watoto wao kwakuzingatia uzuri wa majina hayo, wengine huwapa majina ya wazazi wao, au watu wa ukoo wao ikiwa ni ishara ya ukumbusho, lakini nchini Uingereza Majina haya yameshamiri sana.Jina Noah limeingia kwenye orodha ya majina 10 mashuhuri zaidi kwa kupewa watoto wavulana kwa mara ya kwanza, huku Amelia likisalia kuwa jina ambalo wazazi wengi wanawapa watoto wasichana England na Wales, taasisi ya taifa ya Takwimu Uingereza imethibitisha hilo.
Jina Oliver ndio linaloongoza upande wa wavulana, likishikilia nafasi ya kwanza tangu 2013 nalo Amelia likiwa juu kwa wasichana tangu 2011, Watoto walioitwa Oliver mwaka 2015 ni 6,941 na Amelia 5,158.
Maafisa wa ONS waliorodhesha majina kando kwa mujibu wa jinsi jina lilivyo andikwa, Iwapo majina yanayotamkwa kwa njia sawa yangewekwa pamoja, basi orodha hiyo huenda ingelikuwa tofauti kidogo.
Mfano ni jina Muhammad ambalo linashikilia nafasi ya 12 likiwa na watoto 3,730 ambapo kuna wazazi walioandika jina hilo kama Mohammed (2,332) na wengine kama Mohammad (976),Iwapo majina hayo yangejumlishwa, basi jina hilo lingelikuwa katika 10 bora.


ConversionConversion