Polisi katika ya kaunti ya Kisumu wamemkamata jamaa mmoja ambaye amekuwa akitengeneza pesa bandiaWakaazi wa mtaa wa Nubian katika kaunti ya Kisumu walishangazwa na kijana aliyemshtaki babake kwa kosa la kujihusisha katika biashara ya kutengeneza pesa bandia.
Aidha, kijana huyo alimlaumu babake kwa kususia kutekeleza majukumu yake kama baba mzazi.
Edward Dimba alishikwa na polisi wa utawala akiwa nyumbani kwake na kupatikana na pesa hizo bandia ambazo anazozitumia kuwalaghai watu.

Dima akiwa mikononi mwa polisi
Tukio hilo liliwashangaza wakaazi wa eneo hilo, huku wengi wakistaajabu ya mwana kumsaliti baba mzazi.
Kulingana na kijana huyo Dimba amekuwa akikamatwa mara kwa mara lakini angewachiliwa huru na polisi ambao ni marafiki wake.
“Baba yangu amekuwa akiwaibia watu waliookuwa wakija nyumbani kwetu wakitaka kujua iwapo anatengeneza pesa. Nina dada aliye katika kidato cha tatu na mwingine katika shule ya chekechea, wote wanahitaji usaidizi wangu licha ya pesa kidogo ninayo pata, naitumia pikipiki ya kukodesha, Ksh 300 kila siku.” Alisema.

Edward Dimba amekuwa akitengeza pesa bandia kwa muda sasa
Kijana huyo vile vile alisema kuwa Mamake alipoteza kazi yake na hivyo basi alilazimika kuacha masomo yake na kuanza biashara ya kuendesha piki piki ili kusaidia familia yao.
Polisi walipata pesa bandia na mashine iliyokuwa ikitumiwa kutengeneza pesa hizo kwenye nyumba ya mshukiwa huyo.


ConversionConversion