Wachimbaji wadogo kumi wa madini wanasurika kifo Mererani wilayani Simanjiro


.Wachimbaji wadogo kumi wa madini ya Tanzanite wamenusurika kifo chini ya mgodi wa kampuni ya Tanzani One Mererani wilayani Simanjiro baada ya kuingia kwenye machimbo hayo kupitia njia za panya wakiwa na lengo la kuiba madini.

Mkuu wa kitengo cha ulinzi kwenye kampuni ya Tanzanite One Abubakari Lombe amesema watu hao waligundulika baada ya kuzidiwa na hewa chafu chini ya mgodi na kulazimika kupiga kelele za kuomba msaada ndipo walinzi wa kampuini wakawasikia na wakawasha mashine za hewa safi hili kuokoa uhai wao lakini baadhi yao walikutwa na hali mbaya baada ya kukosa hewa kwa muda mrefu.

Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Tanzanite One Faisal Shahibai ameiomba wizara ya nishati na madini iharakishe utekelezaji wa mpango wa kuweka mipaka sahihi kwenye migodi hiyo hili kupunguza mwingiliano na tabia ya wizi wa madini chini ya migodi inayo sababisha migogoro isiyo ya lazima kati ya wachimbaji wadogo na wawekezaji.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Francis Masawe amethibisha kutokea kwa tukio hilo akisema baada ya kupata taarifa jeshi la polisi lilifanya zoezi la uokoaji hili kuokoa uhai wa watu hao lakini baadhi yao walifanikiwa kutoroka baada ya kuokolewa na wengine wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano
Previous
Next Post »