Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Adelhelm Meru amesema Serikali imejipanga kufikia kwenye uchumi wa viwanda na kuwataka wenye viwanda vya kati kutumia fursa zilizopo kukuza biashara.Akizungumza juzi usiku katika utoaji wa tuzo kwa kampuni 100 za kiwango cha kati, Dk Meru alizitaka kampuni hizo kufanya tafiti na ubunifu katika uzalishaji wa bidhaa zao.
“Nimejifunza kuwa washindi katika tuzo hizi ni wale wenye uongozi bora katika kampuni zao na wamefanya utafiti wa kutosha.
“Kufanikiwa kwa kampuni hizi kunasaidia kuongeza mapato ya Serikali na kuongeza ajira kwa wananchi,” alisema Dk Meru aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.


ConversionConversion