Tiketi za kielektroniki kuanzia kwa Simba, Yanga


Tiketi za kielektroniki zitaanza kutumika rasmi katika mchezo wa mahasimu wa soka nchini Simba na Yanga Oktoba Mosi mwaka huu.

Akizungumza jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema tiketi hizo zitafanyiwa majaribio katika mchezo wa Septemba 25 ambao utakutanisha wabunge wa Simba na Yanga.

“Kuna mechi za kirafiki kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, itakutanisha Bongo Movie na Bongo Fleva, Wabunge wa Simba na Yanga na tiketi za elektroniki ndio tutazifanyia majaribio kwa mara ya kwanza katika michezo hiyo.

“Kila kitu kimekamilika na baada ya majaribio hayo, kuanzia pambano la Simba na Yanga tiketi hizo zitaanza kutumika rasmi na zitasaidia kuminya mianya ya 'wapigaji' wa mapato ya milangoni kwani yameibwa kwa kipindi kirefu sana,” alisisitiza Nape.
Previous
Next Post »