Mkapa afanikisha kurejesha wakimbizi 150 Burundi


JUHUDI za Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, za kufanya mazungumzo ya kurejesha amani nchini Burundi, zimeanza kuzaa matunda baada ya wakimbizi 150 waliokuwa kwenye makambi nchini Tanzania, kuomba kurejea makwao.



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali (mstaafu) Projest Rwegasira, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida, kukabidhi msaada wa vyakula tani 1,800 vyenye thamani ya Dola milioni 1.8 za Marekani (sawa na Sh. bilioni 39.6) kwa wakimbizi.

Msaada huo ulikabidhiwa kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ambao utawanufaisha zaidi ya wakimbizi 200,000 waliopo Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania.

Previous
Next Post »