Mshukiwa wa shambulio New York alisifu Islamic State




Ahmad Khan Rahami alijeruhiwa wakati wa kukamatwa

Waendesha mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka Ahmad Khan Ramani kwa kutega mabomu huko New York na New Jersey mwishoni mwa wiki ambapo mlipuko mmoja ulijeruhi watu 31.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw Rahami ambaye ni mhamiaji kutoka Afghanistan, alinunua vifaa na vitu vya kuunda bomu kupitia kwa mtandao na kuandika makala akilisifu kundi la Islamic State.


Ulinzi umeendelea kuimarishwa jijini New York

Pia ameshtakiwa kwa kujaribu kuwaua polisi wakati akikamatwa siku ya Jumatatu.

Shirika la ujasusi la marekani FBI linasema kwa lilimchunguza Rahami mwaka 2014 lakini halikumpata na chochote cha kumhusisha na ugaidi wakati huo.

Watu 29 walijeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea mtaa wa Chelsea, New York. Kilipuzi ambacho hakikuwa kimelipuka kilipatikana hapo karibu.

Vilipuzi vingine kadha vilikuwa vimepatikana New Jersey siku za hivi karibuni.

Tuyajuayo kufikia sasa:

Ahmad Kham Rahami alikamatwa kuhusiana na milipuko ya New York na New Jersey

Ni raia wa Marekani mzaliwa wa Afghanistan

Anakabiliwa na mashtaka matano ya kujaribu kuwaua maafisa wa polisi, lakini hakuna mashtaka yoyote yanayohusiana na ulipuaji kufikia sasa

Anakabiliwa pia na mashtaka ya kutega mabomu New York na New Jersey

Waendesha mashtaka wanasema aliandika makala akilisifu kundi linalojiita Islamic State
Previous
Next Post »