Msigwa akabidhi madawati 500



Mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa

Mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amekabidhi madawati 537 kwa shule zilizo katika jimbo alke.

Amesema ameyatoa madawati hayo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya madawati hadi kusababisha wanafunzi wengi kukaa sakafuni.

Msigwa amewataka viongozi wa manispaa ya Iringa kuacha tabia ya kuhujumu na kuiharibu miundombinu ya shule na badala yake wahakikishe wanatunza mali zote za serikali kwa lengo la kuweza kuwasaidia vizazi vijavyo.

“Sipendi kuona wanafunzi wanaosoma katika shule za jimbo langu wanakaa chini,kitendo hicho huwa kinaniumiza sana ndio maana nimeamua kupambana kutafuta madawati ili kufanikisha adhima yangu ya kukuza elimu kwa wanafunzi wa jimbo la Iringa mjini”amesema Msigwa

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe amesema kwamba kwa sasa hawana mapungufu yoyote ya madawati hivyo hakutakuwa na changamoto ya mwanafunzi kusoma akiwa sakafuni.
Previous
Next Post »