
Mwalimu huyo alisepa baada ya kupatwa na wakaanzi wa eneo hilo
Mwalimu mkuu wa shule moja katika kaunti ya Bungoma anatafutwa na polisi baada ya kupatikana akishiriki ngono na msichana wa umri wa miaka 12
Maafisa wa polisi wanamtafuta mwalimu mkuu katika kaunti ya Bungoma ambaye ameenda mafichoni baada ya kupatikana akifanya mapenzi na msichana wa umri mdogo.
Samuel Masafu Kongoni , mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Lugusi katika eneo la Webuye, alipatikana afisini mwake akitekeleza kitendo hicho.
Kongoni anasemekana kumtuma msichana huyo dukani siku ya Jumamosi, Septemba, 17 na aliporudi, mwalimu huyo alifunga mlango wa afisi yake na kumnajisi.

Msichana huyo alipelekwa hospitalini ambapo alipatikana kuwa na uja uzito wa mwezi mmoja.
Wakaazi wa eneo hilo waliokuwa shambani wakivuna mahindi waligadhabishwa na kitendo hicho na kuuvunja mlango wa afisi ya mwalimu huyo.


ConversionConversion