Nape apokea 10 milioni za maafa ya Kagera



Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amepokea Sh10 milioni kutoka kampuni ya ujenzi ya Skol Building Contractors kwa ajili ya kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Nape ameishukuru kampuni hiyo iliyowakilishwa na mwenyekiti wake, Vincent Massawe na kutoa wito kwa watu wengine kujitoa katika kuwachangia wahanga wa tetemeko huko Kagera.

Harambee ya kuchangisha michango kwa ajili ya maaafa hayo itafanyika saa 10 jioni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Previous
Next Post »