NIDA kuendelea na zoezi la usajili na utoaji vitambulisho Octoba 3


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kuanza tena zoezi la usajili na utoaji wa utambulisho na Vitambulisho vya Taifa tarehe 3 Octoba ambapo lengo ni hadi kufikia june 30 mwakani Watanzania wote wawe wamepata vitambulisho vya taifa na zoezi hilo linaanza na watumishi wa umma huku vile vya awali vinavyodaiwa kuwa na mapungufu vikirekebishwa baada ya zoezi hilo kukamilika.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mifumo ya TEHAMA NIDA Bw Mohamed Hamisi kwenye kikao cha Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora na waandishi wa habari kilichofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema Desemba mwaka huu kila Mtanzania atakuwa na namba ya utambulisho na baadae kitambulisho.

Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora Mh Angellah Kairuki amesema zoezi hilo litaendeshwa na NIDA kwa kushirikiana na ofisi yake lengo likiwa ni kuhakikisha uwepo wa taarifa sahihi za watu wakiwemo watumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi wake pamoja na kuendelea kubaini watumishi hewa.
Previous
Next Post »