Waathirika wa kimbunga waanza kupokea misaada wilayani Sumbawanga.


Serikali mkoani Rukwa imeanza kutoa misaada kwa wananchi wa kijiji cha Mtimbwa,kilichoko katika wilaya ya Sumbawanga, waliokumbwa na balaa la kimbunga na mvua kubwa ya mawe hivi karibuni,na kusababisha nyumba 27 kuharibika vibaya kwa kuezuliwa mapaa na kubomoka,kwa kuwapa mabati,mbao na misumari ya aina mbalimbali,ili waathiriwa hao waweze kurejea katika hali yao ya kawaida.

Licha ya wananchi hao wa kijiji cha Mtimbwa kwenye Manispaa ya Sumbawanga, kuishukuru serikali kwa msaada huo ambao utawasaidia kujikimu,lakini pia wameiomba serikali iwahudumie wote walioathiriwa na janga hilo bila ya kuwabagua wala kuchakachua majina yao,na kuziomba pia taasisi nyingine kujitokeza kuwasaidia ili waweze kurejea kwenye makazi yao badala ya kujibanza kwa ndugu,jamaa na majirani.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bw Hamidu Masare,akikabidhi misaada hiyo ya vifaa vya kuezekea vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne,amesema wamepanga kutoa misaada kwa awamu kwa kuanzia na wale ambao nyumba zao ziliezuliwa mapaa.
Previous
Next Post »