Rais Magufuli afunguka tetemeko la ardhi Kagera


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema serikali itahakikisha inarekebisha miundombinu iliyoharibika mkoani Kagera kutokana na tetemeko la ardhi, lakini akawataka wakazi ambao nyumba zao zimebomoka wajipange.

Hadi sasa, tetemeko hilo lililotokea Septemba 10 na kuua watu 17 limeshaangusha nyumba 2063, wakati nyingine 14,081 zipo katika hali hatarishi kutokana na kuwa na nyufa na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo.

Tetemeko hilo la ukubwa wa richa 5.7 limeacha watu 126,315 wakihitaji misaada ya chakula, malazi, nguo na mahitaji mengine muhimu.
Previous
Next Post »