Ruvuma yapunguza vifo vya wajawazito, watoto


Tunduru. Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, imepunguza vifo vya wajawazito kutoka 133 kwa wajawazito 1,000 waliojifungua mwaka 2013 hadi kufikia 55 mwaka jana.

Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Alex Kazura alisema mwaka 2013 wajawazito 132 kati ya 1,000 walifariki dunia kutokana na sababu kadhaa, zikiwamo kutokwa damu nyingi, kupasuka kizazi na kuchelewa kufika hospitalini.

Alisema mwaka 2014 iliongezeka na kuwa 133. “Mwaka 2015 idadi ya vifo ilishuka kwa kasi zaidi ya mara mbili na kufikia wajawazito 55 kati ya 1,000 waliojifungua,” alisema.

Kuhusu vifo vya watoto wachanga, Dk Kazura alisema vimepungua kutoka saba hadi kimoja kati ya watoto wachanga 1,000 kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Previous
Next Post »