Serikali kuongeza udhibiti wa matumizi ya tumbaku kuanzia Octoba.


Serikali imesema kuanzia mwezi wa kumi itaongeza udhibiti wa matumizi ya tumbaku kwa kuwaagiza watengezaji wa bidhaa hiyo kuweka matangazo yenye kuonyesha picha ya kifo ya mtu anayevuta sigara ili kupunguza ongezeko la magonjwa yasiyokuwa ya kumbukiza ambayo kwa sasa serikali imekiri yanazidi kuongezeka kila kukicha.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii,jinsi wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu wakati akipokea maandamano ya watu mbalimbali walijitokea kuja kupima magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ambapo watu zaidi ya 2000 wanaratajiwa kuangaliwa afya zao kwa kipindi cha siku tatu.

Naye Mganga mkuu wa Manispa ya Ilala Dk Victoria Ludovick amesema katika tafiti mbalimbali walizofanya zimeonyesha kuwa magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza yamezidi kushamiri na jambo kubwa ni watu kubadili mfumo wa maisha.

Kwa upande wake mtaribu wa kambi hiyo Dk Frank Manase amesema kambi kama hiyo inafanyika kwa mara ya tatu ambapo lengo kubwa ni kuwahimiza wananchi kujenga mazoea ya kujali afya zao ili kuweza kukabiliana na magonjwa kabla hayajaleta madhara makubwa mwilini.
Previous
Next Post »