Sharti la Pep Guardiola kwa Toure kama anataka kuichezea Man City


kocha wa Man City ya England Pep Guardiola ameweka wazi kwa nini hamchezeshi kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure, kocha huyo ambaye amejiunga msimu huu akitokea Bayern Munich ameandamwa na maneno kuhusiana na kuonesha dalili za kutomuhitaji nyota huyo.

Guardiola ametoa kauli katika vyombo vya habari kuwa Yaya Toure hawezi kuichezea tena Man City hadi atakapoomba radhi kwa wachezaji wenzake na timu kwa ujumla, kutokana na maneno yaliotolewa na wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk ambaye anamponda Guardiola amemdharirisha Toure kumuacha katika kikosi cha UEFA.

Pep Guardiola alitoa kauli kuwa “Toure ni lazima aombe radhi wachezaji wenzake, inabidi aombe radhi klabu kufuatia maneno yaliotolewa na wakala wake, kama hatofanya hivyo hatocheza” maneno hayo ya Guardiola aliyasema muda mchache baada ya Toure kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya Ivory Coast.
Previous
Next Post »