
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Urlich Matei.
Jeshi la polisi Mkoani Morogoro linawashikiliwa watu wanne wilaya Mvomero mkoani humo kwa kuvamia kituo cha polisi baada ya mtuhumiwa mmoja kutolewa nje kwa dhamana na baadaye kufariki dunia.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Urlich Matei tukio hilo limetokea jana mchana baada ya kundi kubwa la watu kuvamia kituo hicho cha Mzumbe na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya ambapo watu wawili walijeruhiwa kwa risasi.
Kamanda Matei amewataja watuhumiwa hao waliokamatwa kuwa ni Mohamed Salum, Hussein Juma, Majaliwa Msafiri na Leticia Alex wote wakiwa ni wakazi wa Changarawe wilani Mvomero.
Kamanda Matei ameongeza kuwa watu hao ambao waliipeleka maiti hiyo kwenye kituo cha polisi badala ya hospitali kwa madai kuwa polisi ndiyo wanajua sababu ya kifo cha mtuhumiwa huyo walijiunga kikundi ili kufanya uhalifu katika kituo hicho.


ConversionConversion