JESHI la polisi mkoa wa Kigoma limefanikiwa kuua jambazi sugu aliyekuwa akihusika na mtandao wa matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo wilaya ya Uvinza mkoa wa Kigoma, Wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera pamoja na Mwanza sanjari na kukamata silaha moja aina ya SMG magazine saba na risasi 275 .
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 4:00 asubuhi katika Kitongoji cha Lugongoni baada ya askari kupata taarifa ya kuwepo kwa jambazi anayejiandaa kufanya uhalifu katika maeneo ya Wilaya ya Uvinza Mkoani wa Kigoma.
Alihojiwa na askari ambapo alitoa taarifa ya kuwepo kwa silaha aliyokuwa akitumiwa katika matukio mbalimbali ya uhalifu


ConversionConversion