SERIKALI katika mamlaka ya mji mdogo wa Vwawa, wilayani Mbozi imewatahadharisha baadhi ya watu wanaoozesha au kuoa watoto chini ya miaka 18 kuwa sheria mpya itawakomesha.Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na viongozi wa serikali kwenye mkutano wa kiserikali uliofanyika kwenye uwanja wa CCM wilayani humo, ikiwa ni pamoja na kupokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi ikiwamo kuzungumzia sheria hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa, Japhet Asunga (CCM), alisema kutokana na kukithiri kwa mimba za utotoni zinazosababisha watoto kushindwa kuendelea na masomo na wengine kuolewa na umri huo, serikali imeamua ukomesha hali hiyo kwa kutunga sheria mpya.
Alisema sheria hiyo mpya, mtu akioa mtoto chini ya miaka 18 atakuwa ametenda kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela au faini ya Shilingi milioni tano au vyote kwa pamoja na aliyepokea mahari pamoja na mshenga watapewa adhabu kama hiyo.
Source: Nipashe


ConversionConversion