Zitto Vs Zungu walivyopambana Facebook kwa hoja





HOJA YA ZITTO KABWE NI HII

Moja ya msingi Mkuu wa sera ya mambo ya Nje ya Tanzania Ni kusimama upande wa wanyonge popote walipo duniani. Kutokana Na msingi huu Tanzania imekuwa bega Kwa bega Na watu wa Sahara Magharibi ( POLISARIO ) Na Palestine ( PLO ).


Kumekuwa Na juhudi kubwa ya Mataifa mbalimbali ya Afrika kuondoa utambuzi wake wa Jamhuri ya Sahrawi ( SADR ) hata kufunga Balozi za Nchi hiyo kwenye Nchi hizo za Afrika. Yote haya yanafanywa Kwa msaada mkubwa wa Nchi ya Morocco ambayo inaikalia Kwa mabavu Jamhuri ya Sahrawi.


Morocco imekuwa ikifanya kampeni zake hapa Tanzania Pia. Wanasiasa kadhaa wamekuwa wakikirimiwa na Ufalme wa Morocco na kujaribu mara kadhaa kupenyeza ajenda ya Morocco kwamba Sahara Magharibi Ni sehemu ya Morocco na hivyo Tanzania iondoe kuitambua kwake SADR na kuiondoa kwenye kiti chake Umoja wa Afrika. Habari zilizopo kwenye 'corridors' za kidiplomasia zinaonyesha kuwa Mfalme wa Morocco atakuwa mgeni wa Rais wetu ndani ya Siku chache zijazo.


Wanaohusika Na mipango ya kuvunja msingi Mkuu wa sera ya mambo ya Nje ya Tanzania wakumbuke kwamba UKIJARIBU KUVUNJA MISINGI, UTAVUNJIKA MWENYEWE. Kinachoitwa diplomasia ya kiuchumi kisiwe kichaka cha kuacha mapambano dhidi ya ukoloni, ugandamizwaji Na ubeberu.


Mwalimu Nyerere alituachia heshima ya kuwa Nchi yenye misingi. Siku tunawapa mgongo watu wa Sahara Magharibi, Mwalimu Nyerere atageuka kaburini alipopumzika. Nasi tutakuwa Taifa la hovyo kama Mataifa mengine Afrika ambayo yanauza utu wao Kwa vipande vya sarafu aka Diplomasia ya Uchumi. Tupo ambao hatutakubali Na hatutokaa kimya.


Mwaka 1965 vijana jeuri wa Tanzania waliandamana kupinga UDI licha ya katazo la Serikali ya Mwalimu Nyerere. Sitashangaa hata kidogo kuona UDI ikijirudia mwaka 2016 mbele ziara hiyo ya Mkuu wa Nchi inayokalia Nchi nyengine Kwa mabavu ( occupying power ).


Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi ina Wajibu wa kuwaeleza Watanzania juu ya msimamo wetu kuhusu Sahara Magharibi vinginevyo Serikali isije kulaumu Vijana wenye ujasiri wa kulinda heshima Na msingi wa Nchi yetu - Sera yetu ya Mambo ya Nje inayosimama Na wanyonge.


Comments zikawa hivi



Zungu Mussa Of all the people Zitto you know better .Morocco haikufukuzwa AU walijiondowa wenyewe baada ya Africa kuwapa Kiti Polisario ,hii ni fursa nzuri ya kuwaweka pamoja na kutatuwa matatizo yao tiari kuna azimio la UN la referendum .Tanzania tunajuwa haki za wa Palestine lakini tuna mahusiano na Israel haimanishi tumeachana na msimamo wetu, Leo asilimia kubwa za nchi zilizo pigana na Israel zina mahusiano hasa nchi za Arabuni.Tanzania inanafasi kubwa ya kuzishawishi pande zote mbili kufikia muafaka wa kuingia kwenye kura za maoni kwa azimio la UN


Zitto Kabwe Kuna kampeni kubwa kuwaondoa SADR katika kiti chao AU. Mpaka Sasa wamebakiza Nchi 6 tu kuweza kufikia lengo Lao hilo. Nasikitika sana Nchi yangu inakwenda kuondoa nguvu yake nyuma ya POLISARIO


Like117 hrs
Zungu Mussa Morocco ilichangia ukombozi wa nchi kusini ya Sahara miaka ya 70

Zitto Kabwe Ndg Zungu wewe ulipokuwa Makamu mkt wa Kamati ya Mambo Nje Ndio mlikuwa mnashughulika Na suala hili. Nakumbuka Kamati yenu ilikwenda Morocco wakati mkt wako Ni Edward Lowasa. Hivi mlijiongeza Na kwenda Sahrawi? Au mliishia Rabbat tu? Hiyo Safari iligharamiwa Na Bunge letu au Serikali ya Morocco?


Zungu Mussa Read again


Zungu Mussa Kamati zote za bunge zina garamiwa na bunge


Zungu Mussa Kamati zote za bunge zina garamiwa na bunge



Previous
Next Post »