Serikali imetangaza kufanya zoezi kubwa la sensa katika kuwatambua wafungwa wenye uwezo wa kufanya kazi ili waweze kutumike sasa kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi za askari wa jeshi la polisi na vikosi mbalimbali katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi, ikiwa ni moja ya mkakati unaolenga kuwaondolea adha kubwa ya makazi inayowakabili hivi sasa maafisa na askari wa majeshi hayo.Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mwigulu Nchemba, ametangaza uamuzi huo mjini Musoma mkoani Mara wakati akizungumza na maafisa na askari wa majeshi ya polisi, magereza, uhamiaji na zima moto mkoani Mara, ambapo amesema hakuna sababu ya nguvu kazi hiyo ya wafungwa kutotumika katika kumaliza tatizo hilo kubwa la makazi.
Hata hivyo waziri huyo mwenye dhamana ya usalama wa raia na mali zao, amewaagiza askari polisi kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia maadili bila kumuonea mtu katika kutenda haki huku akiagiza pia kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali kwa baadhi vijana wanaojihusisha na uhalifu wa mauaji ya visasi hasa kwa kuua wanawake kwa njia za ushirikina vikiwemo vikongwe kwa mikoa ya kanda ya ziwa.
Awali mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa mara dk charles mlingwa,akitoa taarifa kwa waziri mwigulu,amesema pamoja na mkoa kuwa katika hali ya usalama lakini bado unakabiliwa na tatizo kubwa la kilimo cha bangi wilayani tarime.


ConversionConversion